24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

ADEM yawahimiza wadau wa elimu kuchangamkia fursa

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Walimu pamoja na wadau wa Elimu nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na Wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM).

Akizungumza na Mtanzania Digital katika maonyesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo na Habari na Uhusiano wa ADEM, Victoria Luhanga amesema kwa mwaka huu wa masomo wa 2022/2023 wanatarajia kutoa kozi ya Shahada ya uthibiti ubora wa elimu (BGAME).

“Nipende kuwakaribisha wadau wa elimu na walimu kufika katika banda letu ili kujua mambo mbali mbali yanayohusu ADEM, kwa walimu wanaotaka kufanya udahili wa shahada ya uthibiti ubora wa elimu (bqame) ni vyema kutembelea tovuti ya chuo ya www.adem.ac.t ,” amesema Luhanga.

Amesisistiza kuwa kozi wanazozitoa katika chuo hicho ni pamoja na udahili wa wanafunzi wa diploma ya uongozi na usimamizi wa elimu (DEMA) na diploma ya uthibiti ubora wa shule (DSQA).

Ameongeza kuwa chuo kina jukumu kubwa la kuwaandaa walimu ili kuwa viongozi na wasimamizi wa elimu katika ngazi mbali mbali .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles