30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Adele akimbiza kwenye chati za Billboard

Adele.NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Uingereza, Adele Adkins, anamaliza mwaka kwa kushika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard kwa wiki nne.

Katika chati hiyo kulikuwa na albamu 200 ambazo zilikuwa zinashindanishwa, lakini Adele amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye ushindani huo kwa wiki nne.

Mkali huyo wa sauti amesema ni furaha kwake kuona kazi zake zikikubalika na idadi kubwa ya watu duniani na ndiyo maana ameweza kukaa kwa muda mrefu ambapo sio kawaida kutokana na ushindani uliopo.

“Hii ni historia kubwa kwangu kuweza kumaliza mwaka nikiwa nimekaa kwenye chati za Billboard kwa wiki nne mfululizo, naweza kusema mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwangu na kikubwa ni kupambana katika mwaka 2016,” alisema Adele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles