23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Adams achukua nafasi ya Henry Arsenal

Tony Adams.
Tony Adams.

LONDON, ENGLAND

BAADA ya mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry, ambaye alikuwa kocha wa vijana wa timu hiyo kutangaza kujiuzulu, nafasi hiyo imechukuliwa na aliyekuwa nyota wa klabu hiyo, Tony Adams.

Henry ameachana na jukumu la kuwa kocha wa vijana baada ya kupishana kauli na kocha Arsene Wenger, baada ya kocha huyo kumtaka achague moja kati ya ukocha au uchambuzi katika kituo cha Sky Sports.

Henry mbali ya kuwa kocha, lakini aliajiriwa na kituo hicho cha utangazaji huku akiwa kama mchambuzi wa michezo, lakini Wenger alishangazwa kumuona nyota huyo akifanya kazi ya uchambuzi na muda mwingi anautumia kuwafundisha vijana ila siku za mwisho wa wiki anawakosoa wachezaji.

Kauli hiyo ya Wenger ilionekana kumgusa nyota huyo na kuamua kuachana na jukumu la ukocha na kubaki kwenye uchambuzi ambapo katika kazi hiyo analipwa pauni milioni 4 kwa mwaka.

Kutokana na Henry kujiuzulu, nafasi hiyo inachukuliwa na aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo, Adams ambaye aliitumikia Arsenal kwa miaka 19 akiwa kama mchezaji, huku akifunga mabao 32 katika michezo 504 aliyocheza.

Hata hivyo, Henrry ameitakia kila la heri Arsenal ya vijana ikiwa na kocha mpya pamoja na ile ambayo ipo chini ya Wenger.

“Napenda nimshukuru Andries Jonker kwa kunipa nafasi ya kuifundisha Arsenal ya vijana kwa kipindi chote nilichokaa, hata hivyo napenda kumshukuru Arsene Wenger kwa maamuzi yake, hivyo nawatakia kila la heri katika mafanikio ya klabu,” alisema Henry.

Mtandao wa Sky Sports, umedai kwamba Henry atabaki kukumbukwa katika ulimwengu wa soka kutokana na kile ambacho amekifanya katika kipindi chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles