26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Adaiwa kuua mkewe kwa kumchoma kisu

Gurian Adolf na Edith Peter-Sumbawanga

MWALIMU wa Shule ya Msingi Chalantai wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Tabita Mwanyanje (29), anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na maeneo mengine ya mwili na mumewe Frank Galimoshi (30) kwa wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justin Masejo alisema tukio hilo lilitokea Agosti 25, mwaka huu saa 10 usiku ulipozuka mgogoro kati ya wanandoa hao hali aliyodai ilisababisha mwanaume kuchukua uamuzi wa kumuua mkewe.

Alidai kuwa mgogoro ulianza pale ilipoingia meseji ya muamala wa mshahara kwenye simu ya mwanamke, ndipo mumewe alipofikiri ni meseji ya M-Pesa aliyotumiwa na mwanaume mwingine.

Masejo alidai kuwa baada ya kuingia kwa ujumbe huo, mume alihamaki na kisha kuanza kumshushia kipigo mke wake, akachukua kisu na kuanza kumchoma sehemu mbalimbali za mwili.

Alidai baada ya mwanaume kubaini ameua, naye alianza kujijeruhi kwa lengo la kujiua kitu ambacho hakufanikiwa, alikamatwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu, na akipona atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.

Taarifa za awali zimeonyesha ndoa ya mwalimu huyo imekuwa na migogoro ya mara kwa mara, baada ya mwanaume kutomwamini akimtuhumu kuwa na mahusiano na wanaume wengine kitu ambacho kilisababusha ndoa yao kutokuwa na amani kama inavyostahili.

Masejo aliitaka jamii kupenda kusuluhisha migogoro inayotokea kwa kufuata sheria na hata ikibidi kuwatumia viongozi wa dini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles