31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

Adaiwa kumuua mkewe kwa wivu wa mapenzi

Gurian Adolf -Sumbawanga

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka Joseph Kalolo maarufu kwa jina la Mwamba, kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumnyonga kutokana na kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, alisema tukio hilo lilitokea alfajiri ya kuamkia Agosti 10, na alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa kuwa ni Maria Kaozya (30).

Kamanda Masejo alisema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia.

Alidai kwamba muda mrefu sasa mke na mume walikuwa katika mgogoro wa kimapenzi huku mke akihusishwa kushiriki mapenzi na mwanaume mwingine ambaye jina linahifadhiwa.

Kamanda Masejo alisema inadaiwa siku ya tukio mwanaume alirudi usiku na kuanza kumpiga mwanamke huyo hali iliyomsababishia majeraha kadhaa mwilini, lakini kama haitoshi alinyongwa shingoni hadi kufariki dunia.

Alidai kuwa baada ya mtuhumiwa kutenda kosa hilo, aliondoka kuelekea kusikojulikana hadi mmoja wa majirani alipofika nyumbani hapo na kugundua kuwa mwanamke huyo ameuawa.

Alisema baada ya jirani huyo kugundua hilo, alitoa  taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.

Kamanda Masejo alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Katika tukio jingine, mwili wa mtu ambaye bado hajatambulika umekutwa katika eneo la Majengo mjini hapa ukiwa ndani ya pagala.

Mwili wa mtu huyo umekutwa jana nyakati za asubuhi maeneo ya karibu na kilabu ya pombe za kienyeji na haikufahamika mara moja nini kimemsababishia kifo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles