29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Adaiwa kumuua ‘house girl’ wake akimtaka amtajie bwana wa mkewe

 ABDALLAH AMIRI – IGUNGA 

JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, linamshikilia Ezekiel Jonas (37) mkazi wa Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga mjini kwa tuhuma ya kumuua msaidizi wake wa ndani, Ester Mahona (16), akimtaka amweleze mke wake alikuwa anatembea na mwanaume gani. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema tukio hilo lilitokea Mei 5, mwaka huu saa nne usiku katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga mjini. 

Alisema binti huyo alikuwa msaidizi wa ndani wa Jonas na baada ya kutengana na mke wake, alimwita ndani na kumtaka amtajie mwanaume anayetembea na mke wake. 

Kamanda Mwakalukwa alidai kuwa binti huyo aliposema hajui, mtuhumiwa hakuridhika na majibu hayo na hivyo kuanza kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali hadi kusababisha kifo chake. 

Alidai kuwa mtuhumiwa alipoona binti huyo amefariki dunia, alichukua mfuko wa sandarusi na kuuweka mwili wake. “Polisi tulipata taarifa kutoka kwa raia wema wakisema kuna binti anapigwa vibaya na tajiri yake, sisi tulifika eneo la tukio saa nne usiku ambapo tulikuta mtuhumiwa ameshamuua binti huyo huku akiwa amemuweka kwenye mfuko wa sandarusi,” alisema Kamanda Mwakalukwa. 

 Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote akitoa wito kwa taasisi za dini kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuacha tabia ya wivu wa mapenzi na kwamba Jeshi la Polisi haliwezi kudhibiti suala hilo peke yake. 

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Stoo kwa nyakati tofauti walishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwahi katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa, na kwamba kitendo alichokifanya ni cha kiunyama na kuiomba Serikali kuchukua hatu akali dhidi ya watu kama hao. 

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Merchades Magongo, amethibitisha kupokea mwili wa Mahona Mei 5 saa 4:30 alfajiri ambapo baada ya kuufanyia uchunguzi walikabidhiwa ndugu zake juzi kwa mazishi. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles