27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

ACT- Wazalendo yakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kamati Kuu ya chama ACT-Wazalendo nchini Tanzania, imeilekeza Kamati ya Uongozi ya Chama hicho kupendekeza jina la mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha, Kamati hiyo imeazimia kuwaruhusu Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wa chama hicho waliochaguliwa kwenda kukiwakilisha chama na wananchi waliowachagua.

Taarifa hiyo imetoewa leo Jumapili Desemba 6, Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu wakati akitoa maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, Tanzania.

“Mosi kamati kuu ya chama chetu imeazimia wawakilishi wachache kwa maana ya madiwani, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge ambao wametangazwa kushinda waruhusiwe kushiriki kwenye vyombo vyao vya uwakilishi.

“Pili Kamati Kuu ya chama chetu imeridhia chama kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na imeielekeza Kamati ya Uongozi ya chama chetu kupendekeza jina la mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,” amesema Ado.

Novemba 19, mwaka huu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi alisema hakuunda Serikali ya Umoja wa kitaifa (SUK) kwakuwa hadi sasa Chama cha ACT Wazalendo bado wawakilishi wa Chama hicho hakijawasilisha majina ya wajumbe wake wa Baraza la Wawakilishi na kula kiapo.

Alisema msimamo wake bado uko pale pale wa kuendeleza maridhiano na kuendeleza umoja miongoni mwa wazanzibari kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.

“Nikotayari kukutana naye wakati wowote na kuwashirikisha kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ikiwemo kuteua na kulitangaza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais.

“Kwa mujibu wa Katiba ofisi ya Rais imeshapeleka barua  Act Wazalendo na kuwataka kutuma majina ya wawakikishi wao lakini hadi leo(Novemba 19,) bado hawajafanya hivyo,” alisema Dk. Mwinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles