29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

ACT-Wazalendo waomba ufafanuzi kwa Magufuli

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es SalaamNA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

VIJANA wa Chama cha ACT-Wazalendo, wamemtaka Rais Dk. John Magufuli, kutoa ufafanuzi kuhusiana na kauli yake ya kusimamisha mikutano ya  siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo, Bakari Licarpo, alisema kauli ya rais ni msiba mkubwa kwa chama hicho, hali inayosababisha kukiua katika siasa.

Alisema chama hicho ni miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana na kufanikiwa kupata jimbo moja Tanzania nzima.

“Kutokana na kauli ya Rais Magufuli, inatulazimu kufanya mkutano katika jimbo moja tu la Kigoma Kaskazini, huku wananchi wengine wakikosa kujua mwenendo wa chama lakini pia mikakati ya chama kutokana na kuzuiliwa na rais.

Sisi wanangome ya ACT tunasema Rais Magufuli anaenda kukizika chama chetu  kwa sababu  sauti zetu hatuna pa kuzipeleka,” alisema Licarpo.

Alisema inawezekana kauli ya Rais Magufuli haijaeleweka vizuri, hivyo ni vema ukatolewa ufafanuzi wa siasa ili kwenda sambamba na demokrasia ya nchi.

“Kauli ya Rais Magufuli inakiuka sheria na Katiba ya nchi kwa sababu katiba ya nchi inaruhusu wanasiasa kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya siasa, ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri,” alisema.

Licarpo alisema ili viongozi bora wapatikane katika nchi, ni lazima waandaliwe katika siasa ndani ya vyama na ndio sababu ya kuunda kwa umoja wa vijana ndani ya vyama.

Alisema hakuna maendeleo yanayopatikana bila kuzungumza, hivyo  kitendo cha Rais Magufuli kuzuia mikutano ya siasa, ni kurudisha nyuma maendeleo.

Kutokana na katazo hilo, ACT imeazimia kuandika barua kwa kila mwanachama kwa lengo la kumpelekea Rais Magufuli   kuruhusu mikutano hiyo ifanyike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles