25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

ACT Wazalendo wajifungia kupitisha wagombea

 ANDREW MSECHU 

UONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, umeanza vikao vyake maalumu kwa ajili ya kupitisha wagombea wa chama hicho kwa ngazi ya urais na ubunge, na kujadili namna chama hicho kinavyokwenda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,mwaka huu. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalum Seif Sharif Hamad alisema mikutanbo hiyo inaanza na mkutano huo, ukifuatiwa na mkutano wa Halmashauri Kuu na hatimaye mkutano mkuu takaofanyika keshokutwa Agosit 5. “Kikao hiki cha Halmashauri Kuu kinajadili majina yawagombea urais, pia wagombea ubunge ambayo hatimaye yatapelekwa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu na kusha kupelekwa kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya uthibitisho,” alisema. 

Alisema katika mkutano huo, mwanachama mpya, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alikaribishwa kama mgeni maalumu, ambapo pia jina lake lilijadiliwa hasa kwa uamuzi wake wa kuwa ni miongoni mwa waliochukua fomu kuomba kuteuliwa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano. 

Maalim Seif aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili hoa zote kwa uhuru bila woga na kuhakikisha kila jambo linajadiliwa kwa ukamilifu ili kuwe na matokeo maazuri katika maamuzi yao. 

Naibu Mwenyekiti Itikadi, uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Janeth Rithe alisema mkutano Kuu ulianza baada ya wajumbe 45 kati ya 51 kuthibitisha uwepo wao. 

Alisema kikao hicho, ni sehemu ya kuelekea kwenye uchaguzi wa ndani ya chama na suala la kwanza litakuwa kupata mgombea urais wa Jamhuri na mgombea wa urais wa Zanzibar. 

Alisema jambo jingine, ni kuzindua ilani ya uchaguzi mkuu ujao kwa ajili ya miaka mitano ijayo ambayo inatoa matumaini ya nini kitafanyika iwapo watapewa ridhaa nawananchi kuongoza nchi. 

Alisema uzinduzi huo utafanya Agosti 5 mwaka huu, unatoa mwanga kutekeleza na kutimiza kiu ya mabadoiliko na itato majawabu mengi ya matatizo yanayoikabili jamii. 

“Napenda kwuafahamisha kuwa leo (jana) tunafanya mkutano wa Kamati Kuu, kisha utafuatiwa na mkutano wa Halmashauri Kuu na kumalizia mkutano mkuu ambao utahitimisha shughuli ya uteuzi wa ndani wa wagombea wa chama na kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020,” alisema. 

Alisema mwaka 2015, chama hicho kilikuwa na ilani nzuri ambayo ilikuwa ya mfano na kwa wakati huu wameandaa ilani inayotekelezeka. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles