22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

ACT WAZALENDO KUUNGURUMA DIMANI

mama-mghirwa

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, leo anatarajia kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa kugombea kiti cha ubunge katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na nafasi za udiwani katika kata walizosimamisha wagombea.

Kampeni hizo zinatarajiwa kuzinduliwa  katika Kata ya Nkome, mkoani Geita, ambapo chama hicho kimejipanga kugawanyika katika makundi mawili ambapo Mghwira ataongoza kikosi cha kwanza akiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Shaban Mambo.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Hamisi, inaeleza kuwa, ziara yao inaanza leo mkoani Geita, katika Kata ya Nkome, chini ya Mwenyekiti Mghwira.

“Januari Mosi watakuwa Kahama katika Kata ya Isagenhe, Januari 2 watakuwa Dodoma na Januari 3 watakuwa katika Kata ya Ihumwa, Morogoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege,” alisema.

Hamisi alisema viongozi hao watakuwa Dar es Salaam katika Kata ya Kijichi, Januari 4 na baadaye Januari 5 msafara huo utaelekea Zanzibar katika Jimbo la Dimani.

Alisema kampeni itaongozwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na Naibu Katibu Mkuu Bara, Msafiri Mtemelwa katika Kata ya Kijichi, Dar es Salaam.

Alisema viongozi hao pia watafanya kampeni hizo Januari mkoani Morogoro, katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, wakati Januari 3 wataunguruma Ruvuma katika Kata ya Tanga.

“Januari nne watakuwa Dodoma katika Kata ya Ihumwa, Januari tano watakuwa Kahama katika Kata ya Isagenhe na kumalizia mkoani Geita katika Kata ya Nkome siku inayofuata,” alisema Hamisi.

Alisema chama hicho kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo waliyosimamisha wagombea kwa lengo kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika maeneo hayo kwa uzalendo kwa Taifa letu.

“Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kusisitiza kuwa, pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli wahakikishe wanampigia kura mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo,” alisema Hamisi.

Aliwahimiza wanachama na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanakiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles