27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ACT-WAZALENDO KUFANYA MKUTANO WA KIDEMOKRASIA

 NA TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha, Machi 25, Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Ado Shaibu, alisema katika mkutano huo kutafanyika mjadala wa kitaifa kutafakari miaka 50 ya Azimio la Arusha, mafanikio na mapungufu yake.

“Mjadala huo utakuwa ni jukwaa la kutafakari misingi na nafasi ya Azimio la Arusha katika Tanzania ya leo, hivyo wananchi wote wanakaribishwa kuhudhuria,” alisema Shaibu.

Alisema chama hicho kimealika vyama na kufanya mazungumzo na Chama cha Labour cha Uingereza, Economic Freedom Fighter (EFF) cha Afrika Kusini, Die Linke cha Ujerumani na Syriza cha Ugiriki.

“Mkutano huo utajadili pia nafasi ya siasa za kijamaa na za mlengo wa kushoto barani Afrika na duniani katika zama za kukua kwa kasi kwa siasa za mlengo wa kulia,” alisema Shaibu.

Katika hatua nyingine, Chama hicho kimemkumbusha Rais John Magufuli kutoingilia utawala wa sheria.

“Katika kilele cha siku ya sheria duniani, Rais alisema watakaofanya makosa wafungwe siku hiyo hiyo, jambo linalokwenda kinyume na utawala wa sheria kwa mujibu wa Ibara ya 13.6,” alisema Shaibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles