29.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

ACT Wazalendo kufanya mkutano wa demokrasia

Ado Shaibu
Ado Shaibu

NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya Mkutano Mkuu wa Demokrasia Septemba 24 mwaka huu na kuhusisha wanachama, wadau wa siasa na wananchi  kujadili masuala mbalimbali ya nchi.

Chama hicho kimetangaza kufanya mkutano huo licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku mikutano yote ya nje na ndani inayohusu masuala ya siasa kwa kile kilichoelezwa kuwa inaleta uchochezi.

Hata hivyo, hivi karibuni, chama hicho kiliruhusiwa na Jeshi la Polisi kufanya kikao cha kamati kuu kwa kile kilichoelezwa kwamba ilibainika mkutano huo haukuwa na dalili za uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi Uenezi na Mawasiliano, Ado Shaibu, alisema mkutano huo ni utekelezaji wa katiba ya chama na   hautajali kuwapo   makatazo aliyoyaita batili.

“Mkutano Mkuu wa Demokrasia upo kwa mujibu wa katiba yetu ambayo imesajiliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa hivyo tutatekeleza wajibu wetu wa katiba bila kujali makatazo batili,”  alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,581FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles