Na Nora Damian, Mtanzania Digital
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kinatekeleza kwa vitendo lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu (SDG’s) linalohimiza usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha ushiriki sawa wa kisiasa wa wanawake ndani ya chama.
Katika uchaguzi wa chama hicho uliomalizika Machi 7,2024 kumeshuhudiwa wanawake wengi wakichomoza katika nafasi za kuchaguliwa na za kuteuliwa akiwemo Doroth Semu aliyechaguliwa kuwa Kiongozi mkuu.
Akizungumza leo Machi 8,2024 kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema wameamua kutekeleza dhana ya usawa wa kijinsia kwa vitendo kwa kuleta mageuzi ya kiuwakilishi ndani ya chama.
“Tulijiwekea malengo mwaka huu maadhimisho yawe kwa vitendo kwa kueleza umma kazi kubwa iliyofanyika kuhakikisha tunaweka misingi madhubuti ya kikatiba na kuonesha ACT inavyotekeleza kwa vitendo dhana ya ukombozi wa mwanamke.
“Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama taifa tumekweka kwenye katiba wajumbe 24 wa halmashauri kuu asilimia 50 wawe wanawake na asilimia 50 wawe wanaume.
“Dhana ya 50/50 sisi tunaitekeleza kwa vitendo kwa kila kanda wajumbe wawili; mmoja mwanamke na mmoja mwanamume,” amesema Ado.
Aidha amesema wamefanya uteuzi wa wajumbe wa sekretarieti ya chama 15 na kati yao 9 (asilimia 60) ni wanawake na sita ni wanaume asilimia (40).
Katibu Mkuu huyo amesema pia katika bodi ya wadhamini ya chama asilimia 66 ya wajumbe ni wanawake pamoja na viongozi wakuu yaani mwenyekiti na katibu.
Amesema mabadiiko na mageuzi yanaanza ndani ya chama ndiyo maana wanahakikisha kunakuwepo na ushiriki wa kisiasa wa wanawake ndani ya chama.
“Tuna sera ya jinsia imejaa ahadi mbalimbali ambazo chama inazitoa kuhakikisha usawa wa kijinsia, tumeweka ahadi ya kuanzisha dawati la jinsia kuhakikisha kwamba ACT panakuwa ni pahala salama zaidi kufanya siasa kwa wanawake kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania,” amesema.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake 2024 inasema; Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na us