24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ACB yapata faida ya bil 1.2/-

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

BENKI ya Akiba (ACB) imepata faida ya Sh bilioni 1.2 katika nusu ya pili ya mwaka ulioishia Desemba 2018.

Faida hiyo ghafi ni ukuaji wa zaidi ya asilimia 700 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kilichoishia Desemba 2017.

Akizungumza kuhusu matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, Augustine Akowuah, alisema ongezeko hilo lilitokana na ukuaji wa mikopo ambayo ilitolewa kwa wateja 13,200, wengi wakiwa ni wafanyabiashara wadogo na wa kati iliyofikia Sh bilioni 80.

Alisema ubora wa mikopo hiyo ulikuwa mzuri kwenye kipindi hicho kutokana na maboresho ya taratibu za utoaji wake na kwamba wastani wa mikopo chechefu ulikuwa ni asilimia 0.7 hadi kufikia Desemba 2018.

“Ninafarijika sana na matokeo haya ya nusu ya pili ya mwaka jana, mizania ya malengo yetu tangu mwanzo wa mwaka yametusababisha kuwa na mwelekeo mzuri wakati tukifunga mwaka,” alisema Akowuah.

Alisema mikakati mingi waliyojiwekea imeleta mabadiliko kwenye benki hiyo kwa muda mrefu, japokuwa hali haikuwa nzuri mwanzo wa mwaka.

“Katika kipindi cha mwaka 2018, Akiba ilitekeleza mikakati ya kupunguza mikopo chechefu, kuimarisha makusanyo ya madeni sugu na utoaji wa mikopo mipya kwa kuzingatia ubora,” alisema.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, hatua walizozichukua ikiwemo kubadilisha na kupitia majukumu na kazi zililenga zaidi kwenye kuimarisha hatari zinazotokana na ukopeshaji. Alisema matarajio ya benki kwa mwaka 2019 ni kuendelea kuwa na matokeo chanya, kwani wanalenga kujenga maendeleo chanya yaliyopatikana mwaka 2018 ikiwemo jukumu pekee la kusaidia wajasiriamali wadogo na wakati nchini kwa kutumia huduma bora za kifedha

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles