27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ACACIA YASONONESHWA RIPOTI YA MAKINIKIA

Mwenyekiti wa kamati ya pili uchunguzi wa mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro

 

 

Na Mwandishi Wetu,

KAMPUNI ya Acacia imesema imesikitishwa na kushangazwa na matokeo ya ripoti ya pili ya mchanga wa madini iliyowasilisha na Tume kwa Rais Dk. John Magufuli   Ikulu  Dar es Salaam jana.

Taarifa iliyotolewa na Acacia   kupitia tovuti yake, saa chache baada ya ripoti hiyo kusomwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Profesa Nehemiah Osoro, ilisema kampuni hiyo imesikitishwa na ripoti ya kamati ambayo ni historia katika uchumi wan chi hii na mambo ya sheria ya kusafirisha mchanga wa madini.

Kwa mujibu Acacia,   ripoti ya pili imejikita katika matokeo ya ripoti ya kwanza iliyotolewa Mei 24 mwaka huu ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiipinga vikali.

Taarifa hiyo inasema ripoti hiyo ilihusisha matokeo ya sampuli za makotena 44.

Pia Acacia imesema kwa taarifa zake za miaka zaidi ya 20 ni vigumu kupatanisha matokeo hayo ambayo yametaja kiwango kikubwa cha thamani ya zaidi ya mara 10.

Kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa na kamati ya pili hiyo jana,   Acacia haijawahi kutangaza mapato na kulipa kodi kwa kipindi cha miaka mingi ambayo ni mabilioni ya dola za Marekani.

Taarifa ya kampuni pia inadai kwamba ripoti ya pili inaishutumu Acacia kutoonyesha mapato halisi pamoja  kutolipa kodi ya mabilioni ya dola za Marekani.

Kwa matokeo hayo, kamati hiyo imetoa mapendekezo ya kuitaka Acacia ilipe kiasi chote cha kodi inachodaiwa, kufanya mazungumzo ya makubaliano ya uchimbaji wa madini, umiliki wa Serikali katika migodi na muendelezo wa kupiga marufuku usafirishaji nje   mchanga wa madini.

“Acacia inakanusha madai haya mapya na ushahidi wake. Sisi tunafanya biashara kwa viwango vya juu  na kufuata sheria zote za Tanzania.

“Tunarudia tena kwamba tulitangaza kila kitu tulichozalisha katika thamani ya  biashara tangu tulipoanza kazi Tanzania

na tumelipa mirahaba na kodi ya madini tuliyozalisha,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa; “Kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na Serikali  na tunaamini kwamba tuna

malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya  jamii na  uchumi nchini Tanzania.

“Acacia inabakia wazi   kuendeleza mazungumzo na Serikali juu ya suala hili na tunaendelea kutathmini yote yaliyoibuliwa na ripoti,” ilisema Acacia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles