23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Acacia kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

Mwandishi Wetu



 Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania (Acacia), inatarajia kuzindua mashindano ya mbio za baiskeli kwa lengo la kukusanya zaidi ya Sh milioni 340 zitakazotumika kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi yote ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Asa Mwaipopo, Meneja Uboreshaji tija wa kampuni hiyo, Janeth Ruben amesema mashindano hayo wameyapatia jina la ‘Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge’.

Amesema mashindano hayo yatazinduliwa rasmi Oktoba 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo na mashindano yenyewe yataanza Novemba 3, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

“Fedha hizo zitasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia sare na vifaa vingine vya shule ikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali,” amesema.

Aidha, amesema hadi sasa mpango wa CanEducate ulioanza mwaka 2011, umetumia kiasi cha Sh milioni 494 kwa kuwadhamini wanafunzi 3,936, na kuziwezesha kwa njia mbalimbali shule zaidi ya tisa.

Naye Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama, ametoa wito kwa wananchi na makampuni mbalimbali kujitokeza katika mbio hizo na kufadhili mpango huo ili kuiwezesha jamii kupata huduma mbalimbali za kielimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles