29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Abiria washambuliwa kwenye treni Ujerumani

train

BERLIN, UJERUMANI

MTU mmoja aliyekuwa na kisu na shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye treni kusini mwa Ujerumani usiku wa Jumatatu na kuwajeruhi watu wanne kabla kupigwa risasi na polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya tukio hilo.

Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa Facebook, kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata matibabu kutokana mshtuko walioupata.

Polisi wamesema bado hakuna taarifa yoyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani mjini Bavaria, kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye asili ya Afghanistan.

Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia nchini hapa, wakiwamo 150,000 kutoka  Afghanistan.

Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa Kiislamu nchini Ufaransa, kumekuwa na hali ya hofu ya kutokea mashambulizi kama hayo nchini Ujerumani.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna ishara zozote kuwa shambulio hilo lilikuwa la kigaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles