ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Tahmed   kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa  Kenya, wamenusufika kifo baada ya basi hilo kuungua moto katika Kijiji Kwamkonga Tarafa ya Mzindu wilayani Handeni.
Ajali hiyo  ilisababishwa na matairi ya nyuma kuwaka moto.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Leonard Paul   alisema ajali ilitokea jana saa 6.00 mchana katika kijiji hicho kwenye barabara ya Segera –Chalinze.
Alisema ajali hiyo ilihusisha basi   namba T.230 BFT aina ya Hiace ambako baadhi ya mizigo ya abiria hao iliteketea katika tukio hilo.
Kamanda   alisema    basi hilo likiwa katika mwendo wa kawaida lilipofika eneo hilo  matairi ya nyuma yalianza kuwaka moto na ndipo abiria waliposhuka na kulishuhudia liliteketea na baadhi ya mizigo yao.
Aiwataka madereva kuendelea kuwa makini wanapokuwa barabarani   kuepuka   ajali ambazo wanaweza kuziepuka kwa kufuata sheria za usalama barabarani.