33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

ABDU KIBA: SKENDO HAZINA NAFASI KWENYE MUZIKI WANGU

Na SHARIFA MMASI


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdu Kiba, amesema maisha yake ya muziki hayasukumwi na skendo za mitandao ya kijaami, badala yake ataendelea kutumia kipaji chake na kutoa kazi zenye viwango.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kiba alisema wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini.

“Muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu mimi na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndio maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu.

“Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake,” alisema Kiba.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles