22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

ABAKA MTOTO KWA AHADI YA KUMPA ANDAZI

Na Kadama Malunde-Shinyanga


JESHI Polisi mkoani Shinyanga  linamshikilia Amos Meshack (36), mfanyabiashara wa udongo wa pemba, kwa tuhuma za kubaka mtoto wa umri wa miaka tisa, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ndala A Manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo lilitokea juzi  mchana nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, Kata ya Ndala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za  mwili.

Alisema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumwita mtoto kwa ahadi ya kumpatia Sh 200 kwa ajili ya kununulia maandazi.

“Kutokana na ahadi hiyo, mtoto aliingia katika nyumba au kibanda ambacho mtuhumiwa hukitumia kufanyia biashara ndogo ndogo za kufinyanga na kutengeneza udongo wa pemba, alimkamata na kumbaka akimsisitiza asieleze chochote kwa mtu yeyote.

“Hata hivyo, mama mzazi wa mtoto aligundua tukio la kubakwa kwa mwanaye  baada ya kumuona akiwa hana furaha na kuamua kumdadisi,” alisema.

Alisema aligundua mwanae  amebakwa baada ya kuona nguo zake za ndani  zikiwa zimefichwa nyuma ya kitanda, huku akionekana mnyonge.

Alisema baada ya kumhoji  mwanae alidai alibakwa na baba Amani ambaye ni Meshack, na kuwa huo ndiyo mchezo wake wa kila siku.

Alisema wakati akianza uchafu huo, alikuwa akimpatia pipi na safari hii alimnunulia maandazi kisha kumvutia ofisini kwake na kumbaka tena.

“Alipelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kupimwa  na majibu ya daktari yalivyotoka ilibainika amebakwa…mchezo huo amekuwa akifanyiwa kila mara na siyo mara moja,”alisema.

Kamanda Haule  alisema wanamshikilia mtuhumiwa na baada ya uchunguzi   kukamilishwa atafikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles