A$AP Rocky, Travis Scott mambo shwari

0
964

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Rakim Mayers maarufu kwa jina la A$AP Rocky, ameweka wazi kuwa, haoni sababu ya kuendeleza bifu lake na rapa Travis Scott.

Kupitia ukurasa wa Twitter, juzi staa huyo aliwaambia mashabiki hana mpango wa kuendelea kuwa kwenye mgogoro na mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa ‘Highest in the Room’

“Niweke wazi kwamba, mimi na Travis Scott hakuna bifu tena, acha maisha mengine yaendelee, sioni sababu ya kurumbana,” aliandika msanii huyo.

A$AP Rocky aliandika ujumbe huyo ikiwa ni siku chache baada ya Travis Scott kuimba midundo huru kwenye tamasha la Rolling Loud huko New York, ambapo kwenye mistari yake alisema, hamzungumzii msanii yeyote kwenye nyimbo zake na hataki kuwa kwenye mgogoro na mtu, maneno hayo yakamfanya A$AP Rocky aweke bifu hilo pembeni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here