32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kanisa Halisi la MUNGU BABA kuzindua vitabu vitatu

Na FARAJA MASINDE

Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 18, Kiongozi wa Kanisa
Halisi la MUNGU BABA, Baba wa Uzao amesema kuwa
uzinduzi huo unatarajiwa kuanza saa 8 mchana hadi saa 11 jioni.
“Kanisa Halisi la MUNGU BABA tutakuwa na uzinduzi wa vitabu vitatu vinavyofahamika kama ‘Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa yote’ na tunatarajia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo wabunge, taasisi za kidini na za kiraia kuhudhuria kwenye kongamano hili la uzinduzi wa ufahamu huu sababu hili ni suala la maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa.


Viongozi Wakuu wa Serikali na taasisi mbalimbali
zikiwamo za dini na za kiraia wanatarajiwa kuhudhuria katika sherehe ya uzinduzi wa vitabu vitatu vya ‘Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda
mataifa yote’ utakao fanyika Desemba 6, mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Lengo la vitabu hivi ni kuelezea jitihada nzuri ambazo zimekuwa zikifanywa na, Rais Dk. John Magufuli hatua ambayo imeleta mabadiliko makubwa kwenye mfumo mzima wa maisha lakini pia kuonyesha kwamba sasa nuru ipo Tanzania na ndiyo maana maajabu mengi yanazidi kutendeka.
“Kwa sasa ibada haiwezi kuwa ile tuliyozoea ya kwenda kuomba bali ni kufanya kazi ndiyo maana hata kauli mbiu ya serikali imebdilika na kuwa hapa kazi tu na hilo limekuwa likijidhihirisha kwa rais wetu kwani tunamuona kabisa anafanya hayo kwa vitendo,” amesema Baba wa Uzao.

Alisema kwa sasa ni kielelezo kwamba nuru imeshukia Tanzania
kutokana na kuivusha kwenye mambo mbalimbali ikiwamo kuondoka kwa janga la virusi vya corona.
“Mungu huyu aliyetushukia Tanzania hakuna vita tena kwenye nafsi zetu, imekuwa ni nchi ya nuru kwani Tanzania leo imekuwa nuru kutokea nchini kwetu kwenda kwa mataifa mengine sababu sisi ni nchi pekee ambayo hatuna virusi vya corona duniani jambo ambalo lina fanya nchi nyingine kuja kujifunza kwetu na kutushangaa, haya ni maajabu ya Mungu.


“Haya ninayoongea ni sauti ambayo imekuwa ikija
mara kwa mara, hivyo vitabu vinavyokwenda
kuzinduliwa vitaonyesha ni kwa namna gani nuru ipo
Tanzania huku rais wetu akiwa ni kielelezo muhimu,” amesema.

Baba wa Uzao alisema kuwa sasa ni wakati wa watu kufanya kazi kwa kuwa ndiyo tafasri nzuri ya ibada.


“Hata zamani kulikuwa na nyumba za ibada lakini tafasri yake ilikuwa ni kuwajibika kwa kutimiza majukumu yako vyema kama ni kulima basi lima, kama ni kufundisha basi timiza wajibu wako vizuri, hiyo ndiyo tafasri ya ibada, ibada ni kufanya kazi kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles