AVELINE KITOMARY
Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), umeandaa kampeni ya siku tano wenye lengo la kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi vinavyosababishwa na ukosefu wa damu.
Akizungumza na MTANZANIA katika Mahojia maalum Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji damu, Dk. Aveline Ngasa amesema wanatarajia kukusanya chupa 32,700 za damu nchi nzima.
Dk. Aveline amesema ukusanyaji damu huo unaambatana na kampeni iliyoanza jana Septemba 21 hadi 25 kwa kulenga maeneo yote ya mijini na vijijini na kwamba katika kampeni hizo kauli mbiu ni ‘Damu salama Uhai wa mama’.
“Ukosefu wa damu unasababisha vifo vya kinamama ambapo moja ya tatu ya vifo hutokea kwasababu hiyo na ripoti ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ya mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kuna vifo 556 kwa kila kizazi 100,000 na vifo hivyo ni asilimia 18 ya vifo vyote vya wanawake wenye umri chini ya miaka 15-49.
“Mama napoenda kujifungua katika kituo cha afya anaweza kupata shida ya kuvuja damu na akahitaji kuongezewa lakini kama haipo ataongezwa nini? Hii husababisha kupoteza maisha,”amesema Dk Aveline.
Amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujitokeza kuchangia damu na kufikia lengo la ukusanyaji damu katika kampeni hizo.
“Hadi sasa kiasi cha mwitikio sio kidogo watu wanajitokeza kuchangia damu lakini tunataka kufikia matarajio yetu hivyo tutaendelea kuhamasisha watu wajitokezwa zaidi.
“Kila mwaka uhitaji wa damu ni chupa 550,000 hii ni sawa na asilimia moja ya idadi ya watanzania na tumejigawa kwa timu ya Halmashauri 185 wanatakiwa kukusanya chupa 150 kwa kila mmoja,hospitali za kanda chupa 500,timu ya mikoa chupa 150 na timu ya damu salama vituo vya kanda chupa 500,”amesema Dk Aveline.
Dk Aveline alitoa wito kwa jamii kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kufanikisha kampeni hizo.
Safi sana tumepokea mpango huo