27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi afikishwa mahakamani kwa ujambazi

MANENO SELANYIKA NA CASTIN CHOGA (DSJ), DAR ES SALAAM

ASKARI wa Jeshi la Polisi na raia wengine watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za unyang’anyi kwa kutumia bastola.

Mbele ya Hakimu Amalia Mushi, Wakili wa Serikali Masini Musa, aliwataja watuhumiwa hao ni askari E.7879 Koplo (CPL) Uswege (44) wa Kituo cha Polisi Mbezi – Kimara, David Kabadi (23), Kasu Gulam (60) na Hilal Ibrahim (70).

Wakili Musa alidai mahakamani hapo kuwa tukio hilo lilitokea Juni 10 mwaka jana maeneo ya Mbezi Afrikana.

Katika shtaka la kwanza, Musa alidai kuwa watuhumiwa waliiba magari mawili aina ya Toyota Prado na Mitsubishi Canter yote yana thamani ya Sh milioni 95 mali ya Abdul Said.

Musa aliongeza kuwa watuhumiwa kabla ya kufanya tukio hilo walimtishia kwa bastola Shaban Kasim ambaye alikuwa mlinzi katika karakana ya magari hayo.

Katika shtaka la pili, watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya unyang’anyi kwa kutumia silaha ambapo katika maelezo yaliyosomwa na wakili Musa waliiba gari aina ya BMW yenye thamani ya Sh milioni 30 mali ya Jay Madeleka.

Baada ya kusomewa maelezo hayo watuhumiwa walikana mashtaka hayo na upelelezi bado unaendelea.

Mahakama ilisema kuwa shtaka hilo halina dhamana kisheria hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 28 mwaka huu ambapo itatajwa tena kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na watuhumiwa walirudishwa mahabusu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles