26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi malaria yapungua

Mwandishi Wetu- Dodoma

KIWANGO  cha ugonjwa wa Malaria nchini, kimepungua zaidi ya asilimia 50 ndani ya miaka miwili kutoka asilimia  14 mwaka 2015   hadi asilimia  7.3 kwa mwaka 2017.

Hayo yamesemwa  jana  na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Leonard Subi wakati wa kikao kazi cha kanda kinachojumisha,waganga wakuu wa mikoa,wilaya, wafamasia na waratibu wa malaria kutoka kanda tano za mikoa ya Dodoma, Singida,Njombe,Iringa na Morogoro.

Alisema mkutano huo,una lengo la kutathimini utekelezaji wa shughuli za Malaria Kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP).

“Tumedhamiria kuitokomeza na kuondoa kabisa malaria Tanzania na mafanikio yameanza kuonekana kwa kipindi cha miaka 10,mwaka 2010 kiwango cha  kilikuwa asilimia 18, sasa tunaongelea asilimia 7.3”.

Alisema vifo vitokananvyo na ugonjwa huo, vimepungua kwa zaidi ya asilimia 75.

“Tanzania bado tunatajwa kama nchi yenye kiwango kikubwa chenye malaria nchi za Afrika, mojawapo kati ya nchi kumi ila bado tunayo fursa ya kuiondosha,”alisema.

Alisema kama nchi, hivi sana wanataka kuwa na mpango endelevu wa kuondoa ugonjwa huo na utasaidia kuondo kuanzia  viluilui na mbu wapevu.

Kwa upande wa binadamu, Dk. Subi alisema mpango huo,  utataka kila atakayeenda kwenye kituo cha kutoa huduma za afya apimwe na akigundulika apewe  tiba. “Tunataka kila atakayeenda kituo chetu cha huduma apimwe, apate tiba sahii na  baada ya tiba  afuatiliwe mana watu wengi tukiwapatia dozi hakuna anayejua kama mtu kiwango  kimeisha na anaendelea vizuri ili watu katika familia yake wasiambukizwe” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles