26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

DK. BASHIRU AMRITHI KINANA CCM

 

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), imemteua Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Bashiru Ali kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kujaza nafasi iliyoachwa wazi Abdulrahman Kinana aliyeomba kustaafu.

Halmashauri hiyo pia imemteua Raymond Mangwala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Queen Mlozi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Erasto Sima kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya chama hicho.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, kikao ya halmashauri hiyo kilichomalizika leo Ikulu jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli pia imeazimia mapendekezo yote ya Tume ya Rais ya uhakiki wa mali za chama yafanyiwe kazi mara moja na chama chenyewe chini ya Baraza la Wadhamini na Uongozi wa Katibu Mkuu, wenyeviti na makatibu wakuu wa jumuia zake.

Pamoja na mambo mengine, Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe, Abdallah Maulid Diwani amefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili na miiko ya viongozi wa CCM.

“Kikao pia kimetoa karipio kwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya kwa mwenendo usioridhisha, usiolinda maslahi ya nchi na unaokinzana na misingi na miiko ya uongozi na wamewekwa chini ya uangalizi wa kimaadili kwa miezi 18,” imesema taarifa hiyo ya Polepole.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles