33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

COLOMBIA YAELEKEA DURU YA PILI YA UCHAGUZI

BOGOTA, COLOMBIA


MGOMBEA wa Chama cha Kihafidhina, Ivan Duque ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais iliyofanyika juzi, lakini hakupata asilimia 50 ya kura ambayo ingemwezesha kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.

Duque alipata asilimia 39.2 ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa aliyekuwa mwanachama wa kundi la waasi, Gustavo Petro aliyepata asilimia 25 ya kura.

Taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka zinazosimamia uchaguzi nchini Columbia zimeeleza kuwa uchaguzi wa juzi ni wa kwanza kufanyika bila kitisho cha waasi wa FARC, katika kipindi cha takriban nusu karne.

Uitikiaji wa wapigakura ulikuwa wa kiasi cha asilimia 53.2, na umefanyika katika mazingira ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Juan Carlos Galindo ameyataja kuwa ya kawaida kabisa.

Mazingira hayo ya amani yamesifiwa na Rais Juan Manuel Santos anayemaliza muda wake, ingawa makubaliano ya amani aliyoyasaini na waasi wa FARC, yalikuwa kigezo kilichowapa mafanikio wagombea wawili waliofanikiwa kuingia duru ya pili.

Duque ameshinda kupitia jukwaa la ahadi ya kuyaandika upya makubaliano hayo, ambayo anasema yanaliendekeza zaidi kundi la FARC, ambalo liliendesha vita vya uasi kwa miongo kadhaa kabla ya kujigeuza kuwa chama cha siasa.

Hata hivyo, amesema nia yake si kuyasambaratisha makubaliano hayo bali kuhakikisha haki, kuzungumzia ukweli, kuwalipa fidia waathirika wa uasi wa FARC na kukamilisha vifungo vyao jela kulingana na matarajio ya waathirka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles