26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS UHURU ‘AFUNGA MILANGO’

NAIROBI, KENYA

UNAWEZA kusema Rais Uhuru Kenyatta, sasa amefunga milango ya mazungumzo kuhusu utata uliojitokeza kwenye uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26, baada ya kutangaza kuwa hatazungumza na kiongozi wa National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga wala Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.

Rais Kenyatta alitangaza uamuzi wake huo jana asubuhi akiwa Ikulu ya Nairobi alikohutubia vituo vyote vya redio vya FM vya Mlima Kenya.

Katika hotuba yake hiyo, alimtuhumu Odinga kwa ubinafsi hivyo hatakutana naye mpaka hapo uchaguzi wa marudio utakapokuwa umefanyika.

Sambamba na hilo, Rais Kenyetta pia alitangaza kuwa hayuko tayari kukutana na Mwenyekiti wa IEBC, Chebukati kwa sababu hana jambo la kuzungumza naye kwa sasa.

Alisema serikali yake imekwishampa Chebukati kila kitu kinachohitajika kwa tume anayoiongoza vitakavyoiwesha kutekeleza majukumu yake ya kusimamia uchaguzi mkuu wa marudio.

Hata hivyo, Rais Kenyetta alisema yuko tayari kunywa chai na Chebukati iwapo ataamua kumtembelea Ikulu.

“Katiba imetoa mamlaka yote kwa watu na ni watu wanaoamua mwelekeo ambao nchi itachukua kwa kupiga kura Alhamisi. Siyo mimi wala Odinga tunaoweza kuwaamulia wakenya milioni 45.

“Nitakuwa tayari tu kumsikiliza baada ya uchaguzi, si vinginevyo. Kabla ya uchaguzi 2007, Rais Mwai Kibaki aliipeleka nchi katika ukuaji wa uchumi wa asilimia saba. Wakati alipopinga (Raila) ushindi wa Kibaki na kutokea machafuko, nchi yetu ikaangukia katika ukuaji wa asilimia sifuri.

“Baada ya mazungumzo yaliyomwingiza katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alimweka Kibaki katika matatizo kipindi chote cha miaka mitano. Iwapo Kibaki angeruhusiwa kuendelea na ejenda zake baada ya 2007, nina uhakika angeipeleka nchi katika ukuaji wa asilimia 10,” alisema Rais Kenyetta.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa uchaguzi huo iwapo Odinga hatashiriki alisema mwitikio mkubwa wa wafuasi wake utaondoa wasiwasi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles