33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ASKOFU GWAJIMA

Na Kulwa Mzee – Dar es Salaam


ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameachiwa huru katika kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Gwajima aliachiwa huru jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeja baada ya Jamhuri kushindwa kuleta mashahidi.

“Upande wa Jamhuri hamuoneshi kujali,  kwa miezi 14 mmeleta shahidi mmoja kutoa ushahidi,”  alisema.

Kesi hiyo jana ilitakiwa kuendelea kusikilizwa lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo, hawakuwa na shahidi wakaomba wapewe ahirisho jingine.

Baada ya Wakili Maugo kudai hayo, Hakimu Mkeha aliamua kuifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) na kumwachia huru Gwajima.

 

Mkeha alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali kesi, ndani ya miezi 14 umeita shahidi mmoja tu.

Gwajima alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo Aprili 17,  mwaka 2015 na kusomewa shitaka la kumtukana Kardinali Pengo.

Gwajima alikuwa akidaiwa kati ya Machi 16 na 25, 2015, katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi dhidi ya Kardinali Pengo.

Inadaiwa alitamka:  “Mimi Askofu Gwajima nasema askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili Yule.”

Gwajima alikuwa anadaiwa  alitoa maneno hayo yakufadhaisha dhidi ya Askofu Pengo na kwamba yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Baada ya upelelezi kukamilika Julai 21, 2015 alisomewa maelezo ya awali ambapo alikana tuhuma hizo huku akikubali taarifa zake binafsi. Upande wa Jamhuri ulidai utakuwa na mashahidi saba na vielelezo kuthibitisha tuhuma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles