28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

M-Pesa yakusanya laki 4/- kuchangia tetemeko

m-pesaNA MAULI MUYENJWA -DAR ES SALAAM

WATANZANIA wamewachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera hivi karibuni kupitia huduma ya M-Pesa, baada ya kuzinduliwa kupitia Kampeni ya uchangiaji ya ‘Red Alert’ inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza, alisema kati ya fedha hizo zilizochangwa baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya uchangiaji wa waathirika wa tetemeko hilo, Sh milioni 99.51 zilitolewa na kampuni  hiyo na Sh 490,000 zilichangwa na Watanzania  kupitia M-Pesa.

“Kiasi kilichochangwa na wasamaria wema ni shilingi  490,000 na sisi  Vodacom tukatoa shilingi milioni 99.51  ambazo zilijumlimshwa na kupatikana shilingi milioni 100 ambazo hundi yake ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu  Septemba 24, mwaka huu na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, baada ya kampeni ya uchangiaji  kuhitimishwa,” alisema Rwehikiza.

Alisema awali taasisi yake ilipanga kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika hao, lakini kwa kuwa Kamati ya Maafa Bukoba ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa  ilikuwa na uhitaji wa fedha zaidi, tuliona ni bora tukabidhi fedha.

Pamoja na hali hiyo, alitoa wito kwa Watanzania, mashirika na taasisi mbalimbali nchini kuendelea kujitoa katika kuchangia waathirika wa tukio hilo, badala ya kuiachia Serikali pekee kwani bado uhitaji ni mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles