33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Muziki wa injili kuiteka Nzega Jumamosi

NA GEORGE KAYALA

CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita) kimeandaa kongamano kubwa la uimbaji ambalo litaenda sambamba kutoa elimu ya Bima ya Afya na suala la Hakimiliki kwa kazi zao.

Katibu Mwenezi wa chama hicho, Stella Joel, alisema kongamano hilo litafanyika Nzega, mkoani Tabora, katika kanisa la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT) na litaanza Juni 11 na kuhitimishwa Juni 12.

“Lengo ni kuwaweka pamoja wanamuziki wa injili wa Kanda ya Magharibi ambao makao makuu yake yapo Tabora, chama kinafanya ziara na kufanya makongamano nchi nzima ili tuwe na sauti moja na kulinda heshima ya muziki huo, lakini pia kuwawezesha waimbaji kufaidika na fursa kutoka serikali na taasisi za kiserikali,” alisema Stella.

Baadhi ya waimbaji watakaoimba kwenye kongambano hilo ni Rose Muhando, Stella Joel, Madam Rut, Lucy Wilson, Ado Novemba, Kwaya ya Ulyankulu, Mapigano, Kinga Christian, Joshua Makondeko, Tumain Njole, Ulimbaga Mwakatobe, Daniel Kwareli na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles