26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa habari watakiwa kuzingatia sheria

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Tanzania Online Media Alliance (TOMA), imewataka waandishi wa habari za mtandaoni  nchini kujiunga na taasisi hiyo ili kujijenga kitaaluma na kuwa na sekta moja ya waandishi wa mtandaoni yenye sauti moja ya kutetea maslahi yao.

Akizungumza Novemba 22, 2023, jijini Dar es Salaam wakati akifungua mpango mkakati huo Mkurugenzi wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC,), Kenneth Simbaya, amesema kuwa katika kuyafikia malengo ni muhimu waandishi wa habari kufanya kazi kwa manufaa ya umma pamoja na kuzingatia sheria na kanuni hususani katika wakati huu ambao sayansi na teknolojia inakua kwa kasi.

Amesema uzinduzi wa mpango mkakati huo wa mtandao wa waandishi wa habari za mtandaoni umelenga kuwaunganisha wanahabari hao pamoja na kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazoendana na wakati na kuzingatia ubora.

“Sayansi na teknolojia inakua kwa kasi, lazima tuzingatie nidhamu katika kufikisha ujumbe kwa jamii pamoja na kuzingatia weledi na sheria za habari.

“Nazipongeza klabu za waandishi wa habari za mikoa yote kwa jitihada mnazochukua katika kuimarisha zaidi tasnia hii ya habari hususani klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ambako imetoka taasisi hii ya TOMA,”amesema Simbaya.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Freedom House, Daniel Lema amesema kuwa, lengo na kuzindua mpango mkakati huo ni kutoa mwelekeo wa namna ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo kwa miaka mitano ijayo.

“Mtandao huu kwa waandishi wa habari za mtandaoni umelenga kuwaunganisha wanahabari hao  na kuwa na sauti moja na kutetea maslahi yao kote nchini kama sekta moja ya waandishi wa habari za mtandaoni,” amesema Lema.

Aidha ameeleza kuwa tasisis  imelenga kuboresha habari zinazotolewa na waandishi wa habari za mtandaoni kwa kuhakikisha zinahusisha sauti za pembezoni ambazo hazisikiki katika uga huo ikijumuisha makundi mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia.

Mmoja ya wanachama wa taasisi hiyo, William Bundala amesema, uzinduzi huo wa mpango mkakati wa miaka mitano ijayo ni fursa kwa wanahabari za mtandaoni kwa kuwa inawaleta pamoja na kubadilishana uzoefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles