30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kiwanda cha TPC chatumia Bilioni 1.2 kuboresha hospitali yake, wanaingi wapongeza

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Kiwanda cha Sukari TPC Moshi kimetumia zaidi Sh bilioni 1.2 kujenga majengo mapya na kuboresha yaliyopo katika hospitali ya TPC pamoja na kununua vifaa tiba lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwenye ukanda wa tambarare ambayo kunachangamoto.

Akizugumza baada ya uzinduzi wa jengo jipya la huduma kwa wateja la hospitali hiyo, Afisa Utawala wa kiwanda cha TPC, Jafary Ally amesema lengo la kiwanda hicho sambamba na uzalishaji wa sukari ni kutoa huduma kwa jamii inayowazunguka.

Amesema TPC imeamua kuipanua hospitali hiyo kwa awamu na kwa miaka mitano iliyopita imetumia zaidi Sh bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya na kuboresha yaliyopo.

“Hospitali ya TPC ilianza tangu 1945 na kipindi chote hiki imekuwa ikihudumia wafanyakazi na wananchi wanaozunguka kiwanda, hivyo kwa kutambua uhitaji wa huduma za afya na ongezeko la wakazi katika eneo hilo ni takriban 95,000 sasa,” amesema Ally.

Amesema hospitali hiyo imejenga wodi ya daraja la kwanza, wodi maalumu kwa magonjwa ambukizi (Isolation ward), jengo la huduma ya mama na mtoto (RCH), kuboresha wodi zote za akina mama, wanaume na watoto.

Aidha, amesema wamenunua vifaa muhimu vya kutolea huduma ikiwemo gari la wagonjwa pamoja na mashine za Theatre, X-ray na Utra Sound huku vingine ikiwa ni kiti cha huduma ya meno na Ventilator.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa hospitali hiyo imeongeza wataalamu tiba wabobevu huku akibainisha kuwa hospitali hiyo imeanzisha huduma za kibingwa kwa kuajiri madaktari bingwa wawili akiwemo daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, bingwa mifupa na kwamba huduma hiyo itatatolewa hospitalini hapo ambapo tayari jengo limekamilika.

Amesema kiwanda hicho kimefadhili ujenzi wa zahanati tano vijiji vilivyo mbali na TPC vya Mserekia, Loondoto, Mawala, Kirungu, Chemchem na kuboresha zahanati ya Mikocheni.

Upande wake, Mkuu wa wilaya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori amesema hospitali ya TPC inamchango mkubwa katika sekta ya afya na kwakuwekeza katika huduma za jamii.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dk. Samia Suluhu Hasan imetoa fedha nyingi katika kuboresha huduma za afya kwenye Halmashauri ya Wilaya Moshi vijiji na tayari hospitali mpya imejengwa na imeshaanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje,” amesema Makori.

Awali, akizugumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Arusha chini, Leonard Waziri amekishukurukiwanda hicho kuendelea kuwekeza zaidi huduma za kijamii.

Amesema wananchi wa kata hiyo walikuwa wanapata adha kubwa ya huduma za afya na kwamba kuboreshwa kwa hospitali hiyo itasaidia kupata huduma bora na karibu badala kwenda mpaka hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles