30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jubilee yazindua mpango wa Maisha Fiti

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee, imezindua mpango wa ustawi unaitwa ‘Maisha Fiti” unaowawezesha udhibiti afya, kinga na tiba kwa wateja wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo leo Novemba 10, jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Jubilee, Dk. Harold Adamson, amesema kampuni hiyo imekuza ustawi wa kimwili na kiakili kwa wateja wake ili kukabaliana na ongezeko la maambukizi ya magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema mpango huo utaunda jumuiya kwa watumiaji kuwasiliana na wenzao na wataalamu wa matibabu kuhusu masuala mbalimbali.

“Magonjwa yanayohusiana na mtindo wa maisha sio tu huathiri ubora wa maisha ya mtu binafsi lakini pia huweka mzigo mkubwa kwa rasilimali za familia na taifa.

“Shughuli za kimwili, unywaji pombe kupita kiasi na lishe duni zimetambuliwa kuwa sababu kuu za kuongezeka kwa mzigo wa magonjwa,”amesema Dk. Adamson.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni, jamii imeshuhudia kuongezeka kwa magonjwa, hali ambayo inahusishwa moja kwa moja na mtindo wa maisha, hivyo mpango huo unawekeza katika elimu ya afya.

Wakati huo huo kampuni hiyo, imezindua kampeni iliyopewa jina ‘Fanya Lolote kwa Hatua’ ili kuwahamasisha watu kujumuisha mazoezi ya mwili katika maisha yao ya kila siku.

“Kampeni hii itawahimiza watu kufanya shughuli kama vile kutembea, kukimbia au kuendesha baskeli ili kuongeza viwango vya nishati na uchangamfu kwa ujumla na kufanya maisha yawe ya kufurahisha zaidi,”amesema Dk.Adamson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles