26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yakanusha madai GGML ku-blacklist vijana nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

SERIKALI imekanusha uvumi kwamba Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imewa-blacklist vijana ambao wamesitishiwa ajira zao na mgodi huo kwa sababu mbalimbali kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Imesema katika ufuatiliaji uliofanywa, imebaini GGML imeweka utaratibu wa kutunza taarifa za kiutendaji na mienendo ya wafanyakazi wake ikiwemo matendo na matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu ambayo mfanyakazi anakuwa amefanya katika kipindi cha ajira yake.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 8 Septemba 2023 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi wakati akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini, Constatine Kanyasu (CCM).

Kanyasu alihoji iwapo Serikali inatambua utaratibu wa Mgodi wa GGML wa ku-blacklist vijana nchini na ni vijana wangapi wapo blacklisted.

Akiendelea kujibu swali hilo, Katambi amesema katika utaratibu wa kuajiri, kampuni na waajiri karibu wote hufuatilia taarifa za utendaji wa waombaji wa kazi kwa waajiri wao wa awali.

“Hivyo, GGML imekuwa ikitoa taarifa za utendaji na mienendo ya wafanyakazi waliowahi kufanya kazi nao pale inapoombwa kufanya hivyo. Aidha, pamoja na kutoa taarifa hizo, GGML haizuii kwa namna yoyote Mgodi husika kuwaajiri waombaji.

“Nitumie fursa hii kuwataka vijana ambao wana uhakika utumishi wao katika Mgodi wa GGML haukuwa na dosari na wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa black-listed katika Kampuni hiyo kuwasiliana na Ofisi yangu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,” amesema na kuongeza;

“Nichukue nafasi hii kuwasihi vijana wote kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kujiepusha na athari za kuwa kwenye kumbukumbu mbaya za utumishi wao hali inayokwamisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi na kushiriki katika Ujenzi wa Taifa letu,” amesema.

Pamoja na mambo mengine Katambi amesema kama upo  ushahidi wa matendo hayo ya vijana kuwa blacklisted, apewe ushahidi huo ili kuhakikisha haki za watanzania hao zinatendeka kwani serikali ni wajibu wetu kulinda haki pande zote.

Mbali na kuahidi kutembelea mgodi huo, amesema kama mtu alishaaadhibiwa ni kosa kuendelea kutumia adhabu hiyo kumnyima haki ya kuajiriwa pengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles