32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Tehama yasajili Wataalam 1,600

Na Mwandishi wetu,Mtanzania Digital

HADI kufikia Juni 31, 2023 Tume ya Tehama nchini imesajili wataalam wa Tehama 1,600 wanaohudumia nchi nzima na bado zoezi la usajili linaendelea.

Hayo yameelezwa leo Agosti 25,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Tume ya hiyo, Dk. Nkundwe Mwasaga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2023/2024.

Amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika Tehama kwani hapa nchini kampuni mbalimbali zimetengeneza mitaji mikubwa na zinafanya kazi nchi nyingi duniani.

“Na mpaka sasa hapa nchini tumeshawasajili wataalamu 1,600 ambao wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali,”amesema Dk. Mwasaga

Aidha, ametaja mafanikio iliyoyapata ni pamoja na kuanzishwa kwa mradi wa kujengwa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti na wabunifu wa Tehama.

Pia, kuanzisha kituo kimoja cha ubunifu Tehama (Softcentre) Zanzibar, vinne vya Kanda katika majiji ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi na Mbeya kwa ajili ya kuendeleza kampuni changa za TEHAMA na kuendeleza kituo cha Dar es Salaam ili kukuza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidijitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo msimamizi mkuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.

“Ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini,”amesema Msigwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles