32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: TFS inavyonadi utalii wa Ikolojia

*Yasema ni fursa nyingine ya kutazamwa na Watanzania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Utalii inatajwa kama Sekta inayokua kwa kasi nchini. Kumekuwa na aina nyingi za utalii ikiwemo utalii wa wanyamapori, mali kale, maghofu, milima, picha, utalii mazingira au ikolojia na vivutio vingine mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania na kuwavutia watalii wengi duniani.

Utalii wa ikolojia ni zao jipya la utalii nchini ambao unafanyika katika maeneo yaliyo hifadhiwa vizuri au kwenye maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu kwa ajili ya shughuli za utalii.

Utalii ikolojia ni wa tofauti ambapo haujazoeleka kama utalii mwingine. Huu ni utalii wa mazingira unaomfanya mtu aweze kutulia kwa kuangalia miti, kupata hewa safi “physically” anaweza kupunguza msongo wa mawazo kutokana na utalii huo.

Akizungumza na MTANZANIA DIGITAL Mkuu wa Sehemu ya Utangazaji Utalii Ikolojia wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Anna Lawuo anasema TFS imepandisha hadhi misitu 20 ya asilia kuwa misitu ya mazingira asilia ‘Nature forest reserves’ ambapo ndani ya misitu hiyo kuna viumbe na mimea adimu ambavyo havipatikani sehemu nyingine duniani.

Amesema utalii wa ikolojia ni fursa mpya za utalii ambao kitovu chake kikubwa ni kuonyesha mazingira asilia ambayo huota yenyewe tofauti na ya kuoteshwa .

“Utalii ikolojia asilia unaofanywa kwenye misitu unakua kwa kasi tofauti na miaka ya nyuma watu wengi walikuwa bado hawajaujua utalii huu ambao unamfanya mtu ajisikie tofauti, ni utalii ambao hauonekani kama ilivyo wanyamapori na vinginevyo,” anasema Lawuo.

Amesema katika misitu yao wanafanya utalii wa ikolojia hawaruhusu kufanya shughuli zingine isipokuwa utalii tu, wanaendelea kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwa sababu ndio kivutio kikubwa hakuna aina yoyote ya takataka hauruhusiwi kuchukua mdudu au mmea wowote.

“Utalii ikolojia ni zao jipya la utalii nchini ambalo halijulikani na wengi lakini linamanufaa mengi makubwa katika maisha ya binadamu kwasababu kunapatikana kwa utulivwa wa hali ya hewa ambayo kila mmoja wetu anapendelea hali hiyo ndio sehemu pekee unaweza kutulia kwa amani,” amesema.

Amesema kuna misitu ya 23 yenye vivutio vya aina ya mbalimbali ikiwemo maporomoko ya maji ambayo ni ya pili Bara la Afrika yenye urefu wa mita 25 yanapatika hifadhi za Kalambo.

Ameelezea kuhusu msitu wa Pugu una faida nyingi mbali na utalii amesema kuna hewa safi ambayo Dar es Salaam huwezi kupata hewa hiyo.

Lawuo amesema wataendelea kuboresha na kutangaza utalii wa ikolojia nchini ili waweze kutoa hewa safi, maji na makazi bora kwa ajili ya wananchi na wanyamapori kwa sababu wanategemea misitu kwa asilimia kubwa na ni muhimu.

Lawuo ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwendakuwekeza katika maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu hiyo kwa ajili ya shughuli za utalii ikolojia ambapo watalii wakija kutalii wanakosa maeneo ya kupumzika ili waendelee na utalii baada ya mapumiziko

Naye Afisa Msaidizi wa TFS wa Wilaya ya Kisarawe, Regina Mwakifuna amesema safu tatu zimepandisha kuwa hadhi za misitu ambazo ni Pugu Kisarawe, Kazimzimbwi na Vikindu Mkuranga imekuwa msitu mmoja tangu mwaka 2020.

Amesema msitu huo upo ndani ya Wilaya ya Kisarawe na inasimamiwa na mhifadhi wa utalii ikolojia ambao ni msitu asilia na kunapatikana bwawa ambalo wanafanya shughuli za kuendesha mitumbwi kwa watalii na utalii wa picha.

“Katika msitu huu kuna maeneo ya mapango ambapo watu wanafanya matambiko bado wana imani katika matambiko hadi sasa kila mhwisho wa mwaka wanaenda kufanya matambiko kwenye mapango hayo maarufu ‘mzimu wa mavoga’ na wengine kufanya utafiti mbalimbali kwenye mashimo ya popo,” amesema Mwakifuna.

Amesema katika msitu huo kuna utalii wa mimea mbalimbali, mimea miwili ambayo ni Minaki shule ya sekondari ambayo imetokana na mmea huo mmea mpugu, Pugu shule ya sekondari Pugu ambapo imetokana na mmea huo.

Aidha, amesema utalii wa ikolojia umeendelea ambao huwezi kuona kushika wala kusimuliwa.

“Utalii wa ikolojia ukienda kutembelea unakutana na mimea ambayo ni dawa kwenye mwili wa binadamu ambayo ni tofauti na hewa ya Air Condition (AC) unapata oksgeni halisi,” amesema.

Amesema changamoto kubwa kwasasa wananchi wengi jamii ya Afrika bado hawajatambua utalii huo.

Amesema wamejipanga kufanya maboresho vile vitu vinahitajika kwa watalii ikiwemo matenti ya watu 200 kwa sasa hawana.

Mwakifuna amesema wataendelea kutangaza utalii zaidi ambapo hadi mwaka jana watalii wa ndani na nje ya nchi idadi ya waliotembelea utalii huo ni 17,890 na nje ya nchi watalii 400 idadi inaizidi kuongezeka tofauti na mwaka jana.

Amewaomba wadau mbalimbali kuwekeza katika utalii wa ikolojia ikiwemo hoteli, migahawa, sehemu za kuogelea “swimming pool” na vitu vingine ambvyo vinahitajika na ni muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles