24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli akiri ugumu wa kuteau Mawaziri

Na Faraja Masinde

Rais Dk. John Magufuli amesema kazi ni ngumu kwenye kuteua baraza la Mawaziri kutokana na kila mmoja kuwa na vigezo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 16, kwenye hafla ya kuwaapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango iliyofanyika ikulu jijini Dodoma.

“Kwanza ni lazima nikiri kwamba sikuwa na haraka sana ya kuteua baraza la mawaziri na nyie wabunge ni mashahidi kwamba mwaka huu tunawabunge zaidi ya 350 na bado wabunge was nafasi zile 10, sasa sikutaka niteue harakaharaka.

“Na mimi ningeomba wabunge presha mzishushe sababu kazi tuliyoomba hapa ni ubunge wala siyo uwaziri, tulitoka hapa wengine mlikuwa wabunge kwenda kuomba ubunge kwamba tutawatumikia wananchi wetu na tukakabidhiwa ilani ya uchaguzi yenye kurasa 303 sasa mengine yanatoka wapi?,” amehoji Rais Magufuli.

Amesema nafasi za mawaziri na manaibu anauhakia haziwezi kufika 30.

“Hivyo hata ungekuwa wewe unateua ungepata shida kubwa, kwa hiyo ni lazima uangalie jina kwa jina vigezo vingi na muda mwingine unavitafuta ili umtoe sababu haiwezekani ukawa na mawaziri sita ndani ya mkoa mmoja.

“Hivyo kuna vigezo vingi na kazi ni ngumu kwa hiyo lazima uwe na usawa na umtangulize Mungu ili anayestahili usije ukamuonea. Kwa hiyo ninawaomba tu ndugu zangu mnisamehe tu kwamba inachukua muda mrefu,” amesema Rais Magufuli.

Alisema mwaka 2015 kazi ilikuwa ni rahisi sababu wabunge wa CCM walikuwa ni wachache kwa hiyo kazi ya kucheza nao ilikuwa ni rahisi.

“Hawa wawili siyo maarufu sana kuliko wengine miaka ya nyuma niliwambia aidha waende kwenye majimbo au warudi walikotoka wakaenda kwenye majimbo, lakini nikaona sababu nitachewa kuwa na baraza la mawaziri na ninyi wabunge lazima mlipwe mishahara na mambo mengine yaendelee lazima tuwe na waziri wa fedha, ndiyomaana nikaangalia mchango wa Dk. Mpango nikasema ngoja nimrudishe.

“Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje napo hatuwezi tukakosa mtu wa kutusemea tukaendelea kutukanwa watu wanatengeneza majambo yao hawapati majibu kwa sabubu nchi yetu haiwezi kujifungia nikaona Prof. Kabudi naye alimudu nafasi yake nikaona nimrudishe,” amesema Rais Magufuli.

Amesema wapo wengi waliomudu nafasi zako lakini aliona ajiridhishe kwanza nakwamba wasaidizi wake walishampelekea majina lakini hakuwajibu.

“Wizara nyingine zote zinasimama ili nijiridhishe, wapo makatibu wakuu wafanye kazi na wajibu wao. Nitakaa na wenzangu kujadili lakini tutakaa pia na mwenzangu Rais wa Zanzibar kwa hiyo ni suala ambalo hali hitaji haraka.

“Hivyo ni suala ambalo halihitaji haraka, kwa hiyo nawaomba sana wabunge najua maneno ni mengi, kwa kwa waganga nendeni shauli yenu, wengine watawapaka mikosi lakini najua hamuendi,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo rais amewaonya wateule hao kuwa awamu hii kazi itakuwa ngumju zaidi ikilinganishwa na awamu iliyopita lengo likiwa ni kutekeleza dhima ya ‘hapa kazi tu’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles