23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

JPM mgeni rasmi mkutano wa ALAT

BENJAMIN MASESE-MWANZA

 RAIS  Dk.John  Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  leo katika mkutano mkuu wa 35 wa  Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanznaia (ALAT), utafaokafanyika  jijini Mwanza kwa siku tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa ALAT,Gulamhafeez Mukadam alisema mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe na viongozi waalikwa zaidi ya 700, huku mada na changamoto mbalimbali zinazozikabili halmashauri zote zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina.

Alisema mkutano huo ambao wajumbe wake ni wakurugenzi wa halmashauri, mbunge mmoja kwa kila mkoa, madiwani na viongozi wengine  waalikwa, utatoa fursa kwao kuileza Serikali  hali halisi ya namna halmashauri zinavyofanya kazi katika mazingira magumu.

Alisema watatumia nafasi hiyo kuwasilisha kilio chao cha muda mrefu juu ya maslahi ya madiwani  na viongozi wa Serikali za mtaa, wakiwamo wenyeviti na wajumbe.

Alisema halmashauri nyingi zimeyumba kutokana na kukosa vyanzo vipya vya mapato.

“Kumbukeni ALAT, ni umoja wa halmashauri ya miji na majiji, tunapokuja kukutana hivi ni jambo kubwa ndiyo maana tumemwalika Rais Magufuli tumweleze  halisi halisi ilivyo.

“Madiwani tunayo madai mengi,yakiwamo kupandishwa posho zetu, hiki ni kilio cha muda mrefu, hivi sasa halmahauri zimenyang’anywa vyanzo vyake na zinafanya kazi katika mazingira magumu, ingawa lengo la serikali nzuri kwmaba fedha zote zikusanywe pamoja na zitakuwa zikirejeshwa kwetu.

“Utakumbuka posho za madiwani zinalipwa kutokana na fedha za ndani, sasa kama vyanzo vya mapato ndio hivyo tumenyang’anywa sasa inakuwa vigumu madiwani kupata stahiki zao kwa wakati, naweza kusema pendekezo letu ni kutaka mzigi huu ubebwe na serikali kuu, maana huku halmashauri zipo taabani,”alisema. Alisema mkutano huo, utaleta fursa kwa Mkoa wa Mwanza na kuwataka wafanyabishara kuchangamkia mwanya huo waweze kufaidika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles