31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu ataka watendaji ofisini kwake wajiongeze

Elizabeth Joachim,Dar es Salaaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waongeze kasi ili utendaji kazi serikalini na kufikia hatua nzuri.

Majaliwa amesema hayo jana Jumanne Mei 28, Jijini Dodoma, alipokutana na watumishi viongozi wa ofisi yake hafla ya futari.

Amesema utendaji kazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mgumu kwa sababu unahusika na usimamizi wa shughuli nzima za serikali na watendaji wote.

“Sekta yetu ni ngumu kwa sababu sisi ni wasimamizi wa serikalini na watendaji, hivyo tuna wajibu wa kuwaunganisha watendaji wa wizara zote serikalini,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu amesema mwezi wa Ramdhani ni muhimu kwa Waislamu wote kwa sababu ni kipindi ambacho wanakamilisha nguzo muhimu za imani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles