23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mhagama aonya waajiri wanaotelekeza wafanyakazi waliopata majanga

NA ELIUD NGONDO  MBEYA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijna, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama, ameyataka makampuni nchini kuacha tabia ya kuwatelekeza wafanyakazi wao wanapopatwa na majanga wakiwa kazini. Mhagama aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya Wakala ya Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA) Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

 Alisema kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiwaacha wafanyakazi wao na kuvunja mikataba wanapokuwa wamepatwa na ajali hali inayopelekea wahanga hao kuendelea kupata shida wakiwa nyumbani kwao.

Jenista alisema wafanyakazi wanapokuwa wamepatwa na majanga ya kuumia ni wajibu wa kampuni husika kumtibu mtu huyo na kuendelea kufanya naye kazi kwa vile  alipokuwa akifanya kazi ndani ya kampuni hilo alikuwa mzima na familia ilikuwa ikimtegemea.

 “Kuna baadhi ya makampuni nchini yamekuwa na tabia mbaya ya kuwatelekeza wafanyakazi wao wanapokuwa wamepatwa na majanga iwe ya kukuvunjia na kupata ulemavu.

“Hali hiyo haikubali ni lazima kuiga mfano kutoka katika Kampuni ya Shanta ambayo haiwatelekezi wafanyakazi wake.  “Kampuni hii ya Shanta  inafanya kazi ya uchimbaji wa madini ya dhahabu wilayani Songwe mkoani Songwe ingawa kuna upungufu mwingine lakini  imejitahidi kwa kuweza kuwajali wafanyakazi wake kwa kutowatelekeza inapotokea majanga tofauti na  kampuni nyingine,” alisisiteza Jenista.

Hata hivyo Msimamizi idara ya Usalama mahali pa kazi, Ulimboka Tuntufye alisema katika kampuni hiyo viongozi wamekuwa wakizingatia taratibu na Sheria za Ajira kwa watumishi wao wanapoanza kufanya kazi.

Alisema kitendo cha kufanya hivyo imekuwa ni vigumu kwa kampuni kuweza kuwatelekeza wafanyakazi wao wanapokuwa wamepatwa na majanga mbalimbali nadani ya kampuni na kuendelea kunufaika.

 “Kampuni ya Shanta ikitokea bahati ambayo mfanyakazi akipatwa na majanga na akaumia kiasi ambacho anaweza kufanyakazi yoyote ndani ya kampuni tunaendelea kuwa naye kama mtumishi mwenzetu na siyo kumtelekeza baada ya kuumia,” alisema Tuntufye.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Osha, Khadija Mwenda alisema wamekuwa wakifanya ukaguzi maeneo mbalimbali lakini makampuni yaliyo mengi yamekuwa na tabia ya kuwatelekeza na kuwafukuza kazi watumishi waliopatwa na majanga.  

Alisema kitendo hicho kimekuwa ni kero kubwa kwa wafanyakazi ndani ya makampuni kuendelea kuachwa na kuajiriwa wengine ambao nao ikitokea bahati mbaya wakapatwa na mjanga ya kushindwa kuendelea kufanya kazi nao hufukuzwa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles