27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

RPC:Trafiki wala rushwa mtaishia gerezani

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathani Shana amewataka askari wa kikosi cha  usalama barabarani kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwani wakibainika wataishia gerezani.

Amewataka askari hao kuanzia sasa kuanza kuwakamata wale wote wanaowapa rushwa na kwa kufanya hivyo yeye atahakikisha anawasilisha majina yao kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro ili wapandishwe vyeo.

Akizungumza na askari wa kikosi hicho mjini hapa jana,Kamanda Shana alisema tayari amekwishafanya mazungumzo na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, wananchi na viongozi wengine kuhusu suala hilo la rushwa kwa askari wake.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri  mnayoifanya trafiki, nimepewa sifa zenu jana wakati wa kuwaaga watalii kutoka Isarel. Lakini bado yapo malalamiko kidogo ya rushwa.

“Bado kikosi chetu kina askari wachache ambao  wanalalamikiwa kwa vitendo vya rushwa. Niseme kwa dhati hawa hatutawavumilia.

“Yeyote ambaye bado ataendekeleza rushwa hatakuwa naye wewe kama bado unajua unaendeleza vitendo vya rushwa anza kuondoka ili uondoke salama, vinginevyo utaishia gerezani,” alisema RPC Shana.

Katika mkutano huo, akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Joseph Bukumbe, Kamanda Shana aliwataka traffiki hao kunza kujenga utamaduni wa kuwakamata wanaowapa rushwa.

“Lakini na nyinyi kwanini utuhumiwe kula rushwa kwani unakula mwenyewe si kuna mtu anakupa. Nitafurahi kama na nyinyi mkianza kukamata wale wanaowapa rushwa.

“Traffiki atakaye mkamata mtu anayetoa rushwa kwa uwezo wangu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha nitahakikisha anapata zawadi kubwa na cheti

“Kwa kitendo hicho cha sifa kwa kuungana na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. John Magufu kupinga vitendo vya rushwa. Niseme kwa dhati mwenye dhamana ya kutoa vyeo ni IGP nitakwenda kwake nitampigia saluti kwa kumwambia wewe ni jembe na unastahili kupandishwa cheo kwani umekata watu wanaotoa rushwa barabarani.

Aliwataka wamiliki wa magari kuhakikisha magari yao wanayafanyia uchunguzi katika wiki ya usalama barabarani kwani jeshi la polisi mkoani humo halitakuwa na salia mtume.

“Tumeanza na ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi wetu kuanzia leo (jana), hawa ni taifa la leo, haiwezekani

 “Tutakagua magari moja baada ya jingine licha ya magari hayo tutazunguka kukagua daladala zote mjini nyingien haazifanani kabisa na magari ya kubeba abiri,” alisema RPC Shana.

Kuhusu magari ya kubeba mchanga na takataka, Kamanda Shana alisema atakuwa Kamanda wa Polisi wa mwisho duniani kuvumilia magari ya aina hiyo.

“Nitakuwa kamanda wa mwisho duniani kuamini gari linalobeba taka nalo likae kitakataka wamiliki wa magari ya taka yafanyiwe marekebisho makubwa“Gari linalobeba taka lisiwe taka liwe kama alivyomiliki wake,” alisema  Shana.

Mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles