27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SmartLab yawakutanisha wajasiriamali,wawekezaji

Dar es Salaam, Tanzania 

Katika kuwajengea uwezo wajasiriamli nchini, Kampuni ya SmartLab kwa kupitia Jukwaa la Founder to founders’ leo limefanya awamu ya tatu ya makongamano yake yenye lengo la kuwakutanisha wajasiriamali, wamiliki wa makampuni, wawekezaji na wadau mbalimbali.

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano inayoratibiwa na Kampuni ya SmartLab inayowaleta pamoja wavumbuzi mbalimbali na kujengeana uwezo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwanzilishi wa kampuni hiyo ya SmartLab, Edwin Bruno, amesema majadiliano katika jukwaa hilo hulenga kuibua mada mbalimbali ili kupata ufahamu wa jinsi ya kukuza kampuni mpya.

Bruno ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Smart codes Limited amesema mojawapo ya changamoto inayowakabili waanzilishi wa kampuni nchini ni jinsi ya kukuza kiufanisi soko la kampuni husika.

“Founder to founders ni jukwaa kwa ajili ya kampuni mpya kukutana na wawekezaji, waanzilishi wenza na washirika. 

Pia inawawezesha kuungana na kushirikiana wakati wa kubadilishana mawazo ya ubunifu kwa ajili ya kukua, kubadilisha mitazamo na kutengeneza ufumbuzi wa mambo mbalimbali kulingana na mazingira ya kitanzania na Afrika kwa ujumla.

Ameongeza “Kampuni mpya, wajasiriamali, wabunifu na wavumbuzi wa biashara za hapa nyumbani sasa wana sehemu moja ya kukutana na kufanya shuguli ambazo zitakutanisha na kukuza jumuiya za uvumbuzi zilizo tofauti na zenye vipaji hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla kupitia Mwanzilishi kwa Waanzilishi”

Amesema Jukwaa la Founder la founders linatoa muungano wa muhimu ambao unawezesha wajasiriamali na kampuni mpya kujua mienendo mipya kwenye sekta ya uvumbuzi. 

Aidha, Mkurugenzi wa Raha Liquid Telecom, Kumeil Abdulrasul, ambaye ni mdhamini mkuu wa jukwaa hilo, amesema ubunifu ndio hatima ya miaka na kizazi kijacho.

” Ndio maana Raha Liquid Telecom tunajivunia kuwa sehemu ya timu ambayo inataka kubadili hatima ya ubunifu, kampuni mpya na mazingira ya ubunifu Tanzania”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles