Wizara kuja na mbadala wa mazao yanayoozea mashambani

0
1111

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa amesema Wizara yake imepanga kuja na miundombinu itakayowasaidia wakulima kuondokana na adha ya mazao kuozea mashambani.

Ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 4,katika utaiji tiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya mauziano ya mahindi kati ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) uliofanyika Ikulu jijini Dar ES Salaam .

Bashunga amesema mkakati huo una nia ya kuboresha kilimo kwani mbali na kupata changamoto hiyo lakini pia wana changamoto za masoko ya mazao ya kimkakati hivyo kupitia mkataba huo pia wataongea na WFP ili wanunue na mazao megine tofauti na mahindi.

“WFP wanasambaza chakula katika nchi nyingi sana tunataraji kuongea nao ili waje kununua mazao mengine kutoka hapa nchini na kufanya hivyo wakulima watakuwa wamepata soko la uhakika,

“Huu mkataba unaosainiwa leo ni matokeo ya jitihada za wizara yetu kufata maelekezo ya Rais na tunafanya kazi kwa ukaribu na wadau wa kilimo na taasisi za serikali nchini kuhamasisha kilimo cha tija nchini na kuhakikisha wakulima wetu wanapata masoko ya uhakika kwani ndio mkombozi wao,” Naibu waziri wa kilimo Innocent Bashungwa.

Aidhaamaetoa rai kwa viongozi wa vikundi vya wakulima na Bodi za mazao hapa nchini kaucha kujifikiria wao na badala yake wawafikiria wakulima amba ndo wanatumia muda wao na fedha kuwekeza katika kilimo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here