23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Hasunga ataka wakulima wa mazao watambuliwe


NA MWANDISHI WETU -Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za mazao nchini kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo likiwa ni kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yote.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo kwenye Ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Hasunga alisema ili kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuandaa mipango madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua wakulima wote nchini na kuongeza kuwa wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa kwa  wizara yake kufanya jambo kama hilo katika mazao mengine hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, Waziri Hasunga alitoa agizo kwa Bodi ya Korosho kuandaa daftali maalumu la kuwatambua wakulima hao kote nchini ambapo moja ya taarifa ambazo zitajumuishwa katika daftali hilo ni pamoja na jina kamili la mkulima,  mkoa, wilaya, kata na tarafa anayotoka.

Mambo mengine ni pamoja na kitongoji, mtaa au jina la kijijini anapotoka, mahali lilipo shamba pamoja na ukubwa wa shamba lake.

Aidha Waziri Hasunga aliongeza kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe hadi kufikia hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa na mfumo maalumu wa kanzi data ya kuwafahamu ili kushughulikia mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles