31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

NSSF YATOA MSAADA KWA HOSPITALI IRINGA

Na RAYMOND MINJA -IRINGA
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani hapa, umetoa msaada wa shuka 300 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 4.5 kwa Halmashauri na Manispaa ya  Iringa kusaidia upungufu uliokuwapo.

Msaada huo ulikabidhiwa jana na Meneja wa NSSF  Mkoa wa Iringa,  Josephat Komba ambaye alisema kuwa wameutoa ikiwa ni utekelezaji wa maombi
yaliyotolewa na halmashauri hizo kwao.
“NSSF kama mfuko wa hifadhi ya jamii, unalo jukumu la kuendelea kuunga mkono jitihada za halmashauri  nchini katika kutoa huduma za afya, ikiwa ni kuunga  mkono  jitihada za Serikali kuhakikisha huduma za
afya zinaboreshwa ili wananchi wake waweze kupata huduma bora,” alisema.
Komba alisema NSSF itaendelea kuwa karibu na jamii ya Watanzania kwani hatua ya waajiri kuwaunganisha  wafanyakazi wao na mfuko huo, ni kutaka kuona  maisha yao yanaendelea kuboreshwa zaidi, hivyo
jukumu lao ni kuendelea kuunga mkono uboreshaji wa  huduma za afya.
“NSSF imekuwa ikisaidia katika huduma mbalimbali za  kijamii pamoja na kusaidia halmashauri, ila pia  tumekuwa tukisaidia huduma ya matibabu kwa  wanachama wetu bure pamoja na familia zao,” alisisitiza.
Komba aliongeza kuwa Hospitali ya Manispaa ya Iringa, Frelimo iliomba msaada wa kupatiwa shuka 200 na Halmashauri ya Iringa iliomba shuka100.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Omary Mkangama, aliipongeza  NSSF kwa msaada  huo katika Hospitali ya Frelimo na  kuomba ushirikiano huo kuendelea zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles