RAPA 50 Cent amedai kujitoa kwenye mtandao wa Instagram kutokana na baadhi ya mashabiki kufungua akaunti mbalimbali kwa ajili ya kulichafua jina lake.
Bosi huyo wa kundi la G-Unit, amesema kwamba wapo mashabiki wanafungua akaunti za Instagram wakitumia jina la 50 Cent halafu wanaweka picha mbalimbali za ajabu.
“Sioni sababu ya kuendelea kuwa kwenye Instagram kutokana na baadhi ya watu kuutumia vibaya mtandao huo, kuna watu wanafungua akaunti na kuweka picha zangu na mambo mengine ambayo hayana maana yoyote kwa jamii.
“Kuanzia sasa yeyote ambaye ataona picha zangu kwenye Instagram, siyo mimi, ni baadhi ya watu wanaotaka kulichafua jina langu, lakini wafanyakazi wangu ambao ni wataalamu wa kompyuta wanafanya utafiti kuweza kumjua mhusika,” aliandika 50 Cent kwenye akaunti yake ya Twitter.