22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

5 za Jay Dee miaka 20 kwenye Bongo Fleva

Christopher Msekena

MIONGONI mwa majina makubwa yenye heshima ya kipekee katika muziki wa kizazi kipya nchini ni Lady Jay Dee, mmiliki wa majina kibao yaliyobeba hadhi aliyonayo kwenye muzuki alioweza kudumu ndani yake kwa miaka 20 sasa.

Februari 1, mwaka huu Jiji la Dodoma  litapambwa na onyesho la miaka 20 ya Jay Dee kwenye Bongo Fleva huku akisindikizwa na mtoto wake wa kufikia, Karen, washiriki wa Bongo Star Search, Afro Jay na Patrick Alsina katika ukumbi wa Royal Village.

Jay Dee anasema amelichagua Jiji hilo sababu ni makao makuu ya nchi lakini pia baada ya Dodoma maonyesho mengine yatafuata katika mikoa mingine hivyo mashabiki wakae mkao wa kupokea burudani ya nguvu.

Akiwa katika maandalizi ya kuwapa shoo za kibabe mashabiki zake, Swaggaz  tumefanya mahojiano maalum na Jay Dee na tunayaleta kwako kama tano za Jay Dee miaka 20 kwenye muziki.

1

Swaggaz: Katika miaka 20 ya uwepo wako kwenye muziki mambo gani anajivunia?

Jay Dee: Najivunia heshima niliyojijengea na mapenzi kutoka kwa watu wa rika zote pia kutambulika kama mmoja ya wasanii walioikuza Bongo Fleva.

2

Swaggaz: Kuna mambo gani ambayo umeyapitia kwenye muziki na hutaki wanamuziki wengine wachanga hasa wakike wayapitie?

Jay Dee: Hakuna kitu cha ajabu ambacho mtu hawezi kukabiliana nacho na huwezi kuzuia vitu visitokee, changamoto humjenga na kumwimarisha mtu.

3

Swaggaz: Ukiwa kama binadamu kuna makosa gani ambayo umewahi kuyafanya na kuna muda huwa unayajutia?

Jay Dee: Kila binadamu hukosea na mimi nimewahi kukosea mara nyingi sana ila Mwenyezi Mungu pekee ndiyo natakiwa kumtubia na kumwelezea makosa yangu sioni kama ni sahihi kuuelezea umma makosa au majuto yangu, it’s personal (yangu binafsi).

4

Swaggaz: Kwa wanamuziki wakike wapya wanaofanya vizuri sasa, unaona nani anaweza kuvaa viatu vyako kama Malkia wa Bongo Fleva katika nyanja za uwezo kimuziki kujituma, kutokata tamaa na kujipambania. 

Jay Dee: Kila mmoja anajitahidi kwa nafasi yake na siku zote kila mtu huacha alama yake yeye kama yeye, kila mmoja ni ‘special’ hivyo tusimvalishe yeyote kiatu cha mwingine. Hata wao pia tusigawe viatu vyao kwa watakaofuata wavivae.

5

Swaggaz:  Tulipotoka mpaka hapa tulipo, unauonaje muziki wa Bongo Fleva, kuna mambo gani mazuri na mabaya yaliyopo sasa kwenye tasnia?

Jay Dee: Mambo mazuri ni kwamba wanamuziki wanaongezeka na ajira inakua kwa upande huo, mambo mabaya ni kwamba watu kuegemea kwenye makundi ya aina moja hivyo kupelekea wengine wasipate nafasi wanazostahili  pia media (vyombo vya habari) zinafuata mkumbo wa stori badala ya kuegemea kwenye vipaji halisi, media zinaua vipaji.

NYONGEZA

Swaggaz:  Katika albamu zako zote ulizowahi kutoka albamu ipi ilikuwa na mafanikio zaidi?

Jay Dee: Kila albamu ina mafanikio kwa namna yake kwahiyo siwezi kuzilinganisha wala kuzishindanisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles