22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MTINDI UNAVYOSAIDIA MWANAMKE KUJISAFISHA

 

 

KWA kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu ‘Vaginosis’.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanamume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni

• Kuwa na wapenzi wengi

• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango

• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali

• Uchafu

• Uvutaji sigara

• Pombe

• Maambukizi ya bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili

• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida

• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza

• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke

• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu

• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa

• Maumivu makali chini ya kitovu

• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Matibabu

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.

Pia unaweza kutumia dawa za asili zifuatazo:

Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ndiyo dawa ya asili nzuri kuliko zote kwa ajili ya maambukizi ya bakteria kwa wanawake. Kitunguu swaumu ni antibiotiki ya asili na hufanya kazi ya kuua bakteria wasababishao huu uchafu ukeni bila shida yoyote.

Menya punje tatu au tano za kitunguu swaumu, zipondeponde kidogo na uzifunge vizuri ndani ya kitambaa laini na ingiza ndani ya uke wako kwa saa sita hivi kisha ukitoe. Pia menya punje sita za kitunguu swaumu na uzikate vipande vidogo vidogo (chop) na unywe na maji nusu lita asubuhi ukiamka au usiku unapoenda kulala kwa wiki mbili mpaka tatu.

Mtindi

Chukua mtindi ujazo wa kijiko kidogo cha chai na utumbukize ndani ya uke wako na uache huko usiku mzima. Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika ukeni kuweka sawa usawa wa PH (alikalini na asidi) na hivyo kuondoa maambukizi. Pia unashauriwa kula tu huu mtindi mara mbili kwa siku kuongeza kinga ya mwili wako kwa ujumla dhidi ya magonjwa mbalimbali.

3. Siki ya tufaa

Chovya pamba ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na uweke ndani ya uke kwa dakika 15 hadi 20 kila siku na bakteria wabaya wote watakufa.

4. Uwatu

Loweka kijiko kidogo cha mbegu za uwatu (fenugreek seeds) ndani ya maji glasi moja na uache kwa usiku mzima. Kesho yake asubuhi maji haya yaliyolowekwa mbegu za uwatu kabla ya kula au kunywa chochote. Uwatu husaidia kuweka sawa homoni za mwili na kuweka sawa mzunguko wa hedhi.

 

Maziwa na binzari

Changanya kijiko kimoja cha chai cha binzari (manjano) ya unga na kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe mara mbili kila siku mpaka tatizo litakapoisha.

Lemonade

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo

Jinsi ya kuiandaa 

* Chukua asali nusu Lita

* Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji lita tatu, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za limau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita mbili na nusu.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu lita na hiyo juisi ya limau lita mbili na nusu, ongeza maji safi ya kawaida lita mbili ili kupata lemonade ya ujazo wa lita tano. Ihifadhi katika friji.

Kunywa robo lita kutwa mara mbili kwa siku 10 hadi 11.

Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya unga ndani ya hii juisi ya lemonade.

Jeli ya mshubiri (aloe vera jel):

Ingawa jeli halisi ya mshubiri haitibu moja kwa moja tatizo la kutokwa na uchafu ukeni, inaweza kuwa msaada mkubwa katika kupunguza maumivu na muwasho ukeni. Chana kipande kidogo cha jani la mmea huu na ukamue kidogo kupata maji maji yake na upake vizuri taratibu ndani ya uke mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa hadi muwasho utakapoisha.

Mambo ya kuzingatia

Zingatia dawa peke yake hazitofaa kitu bila kuzingatia ushauri au masharti muhimu yafuatayo:

Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi nane hadi 10. Punguza vyakula vyenye wanga,

acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya kuwa rahisi kupata maambukizi ya fangasi.

Epuka kufanya mapenzi kinyume cha maumbile. Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali.

Kuwa na mpenzi mmoja tu, pendelea kujiweka msafi muda wote, oga maji ya moto, acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa. Pia unapaswa kuacha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya ukeni.

Mwandishi wa makala haya ni Fadhili Paulo ambaye pia ni mtaalamu wa dawa asili. Kwa mawasiliano tuma ujumbe wa  WhatsApp+255769142586.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles