WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM AFUTA POSHO ZA MADIWANI DAR ES SALAAM

0
1175

majaliwa-kassim

NA FERDNANDA MBAMILA

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amefuta posho za madiwani wa mkoa wa Dar es Salaam zisizo za kisheria na kuamuru fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Akiwa katika ziara Wilayani Kigamboni, amesema wanaokusanya ushuru ni wengi lakini wanaonufaika na fedha hizo ni wachache.

Wakati huo huo, amegiza kila mkurugenzi wa halmashauri ajue matatizo yanayoikabili halmashauri yake ili fedha zitakapotolewa zilingane na matatizo aliyonayo kulingana na fedha zilizotengwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here